IQNA

Utawala wa Israel unajaribu kuzuia shughuli za Qur'ani katika Msikiti wa Al-Aqsa

13:47 - November 23, 2023
Habari ID: 3477935
AL-QUDS (IQNA) - Utawala wa Kizayuni wa Israel umeweka kwa walimu wa kike wa Qur'ani Tukufu katika Msikiti wa Al-Aqsa huko Al-Quds (Jerusalem).

Vizuizi hivyo vinalenga kukomesha vikao vya qiraa ya Qur'ani Tukufu na darsa za Qur'ani Tukufu katika eneo hilo la tatu kwa utakatifu kwa Waislamu.

Wakihojiwa na Al Jazeera walimu wa kike wa Qur'ani Tukufu wanazungumza kuhusu majaribio yaliyopangwa na Israel ya kuzuia shughuli zao za Qur'ani katika msikiti huo.

Muntaha Abu Sanina, mmoja wa wanawake hao, anasema amejifunza Qur'ani Tukufu n na kupata cheti kinachohitajika cha kufundisha Qur'ani Tukufu.

Vikosi vya Kizayuni vimemkamata na kumhoji mara tatu kwa kufundisha Qur'ani katika Msikiti wa Al-Aqsa.

Abu Sanina anasema Wazayuni walipinga tamko lake Allahu Akbar (Mungu ni mkubwa), wakidai amewatisha walowezi wa Kiisraeli (ambao huingia kinyume cha sheria katika eneo takatifu la Waislamu kila mara) kwa kufanya hivyo.

Zaynab al-Jallad mwalimu mwingine wa Qur'ani Tukufu ambaye amepigwa marufuku kuingia Al-Aqsa na kuhudhuria vikao vya qiraa ya  Qur'ani Tukufu hapo.

Anasema kuna shauku kubwa ya kujifunza Qur'ani Tukufu miongoni mwa vijana wa Kiislamu huko al-Quds na hili limewatia wasiwasi maafisa wa utawala wa Kizayuni.

Kozi za ufundishaji wa Qur'ani Tukufu hutolewa katika Msikiti wa Al-Aqsa katika ngazi tatu kwa lengo la kuinua kizazi kinachofahamu mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

4183483

Habari zinazohusiana
captcha