IQNA

Jinai za Israel

Askari wa Israel Baada azirejesha funguo alizoiba za Msikiti wa Al Aqsa miaka 56 iliyopita

22:15 - May 22, 2023
Habari ID: 3477032
TEHRAN (IQNA)- Mwanajeshi wa zamani wa utawala haramu na wa Kizayuni wa Israel amezirejesha funguo za Babul-Magharibah, moja ya milango ya ukuta wa magharibi wa Msikiti wa Al-Aqsa, tangu alipoziiba miaka 56 iliyopita katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na akaeleza: "hivi ndivyo Israel inapaswa kuwafanyia Wapalestina".
Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Falastin Al-Yaum, katika mkanda wa video uliotolewa na Idara ya Wakfu wa Kiislamu Quds tukufu inayokaliwa kwa mabavu, Yair Barak, mwanajeshi wa zamani wa utawala wa Kizayuni, anaonekana akikabidhi funguo za Msikiti wa Al-Aqsa kwa Sheikh Azzam al-Khatib, mkurugenzi mkuu wa idara hiyo.
 
Katika mkanda huo wa video, Barak anasema wakati akikabidhi funguo za Msikiti wa Al-Aqsa, "baada ya takriban miaka 40 au 50, nimeingiwa na huzuni kuona kwamba ufunguo wa Babul-Magharibah (moja ya milango ya ukuta wa magharibi wa Al- Msikiti wa Aqsa) ningali ninao mimi isivyostahiki kwa sababu niliuiba. Kwa hiyo nimeamua kuurejesha kwa wenyewe".

Mwanajeshi huyo wa Kizayuni ameongeza kuwa, sasa ufunguo huo umerejea kwa wamiliki wake halali na hivyo ndivyo Israel inapaswa kufanya kwa kurudisha ardhi, haki, heshima, kujitawala, uhuru na usalama kwa Wapalestina.

 
Yair Barak ameendelea kueleza kwamba: Baada ya kuurudisha ufunguo kwa wenyewe, ninahisi nimefanya jambo zuri sana, ikiwa ni baada ya kufikiri kwa miaka mingi juu ya kulifanya jambo hili na ninatumai kuwa matokeo ya jambo nililofanya yatakuwa na taathira chanya kwa watu.
 
Askari huyo wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel amezungumzia pia sherehe za kile kinachoitwa "Maandamano ya Bendera" na akasema, siku inayoitwa eti takatifu ya Kiyahudi ni moja ya siku za mwaka zinazochukiza mno. Mimi nimeacha muda mrefu kusherehekea siku hii kwa sababu ni kielelezo cha kuvamiwa na kukaliwa Baitul Muqaddas (Jerusalem) kwa mabavu.

3483656

captcha