IQNA – Kuanzia unyanyasaji wa mtandaoni hadi mashambulizi ya umati na sera za kibaguzi, mwaka 2025 uliweka bayana hali ya kutisha kwa Waislamu walio wachache nchini India.
IQNA- Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa, Jamhuri ya Iran ya Kiislamu ni mbeba bendera ya kukabiliana mfumo wa kibeberu na mlinganiaji wa kuwepo mfumo wa kiadilifu wa Kiislamu ulimwenguni; suala ambalo kwa mujibu wake, ndilo sababu kuu ya mkanganyiko wa mataifa makubwa.
IQNA – Katika aya za Qur’ani Tukufu, Istighfar (kuomba msamaha wa Mwenyezi Mungu) imeelezwa kuwa miongoni mwa masharti ya kuingia Peponi na pia ni ada ya kidunia ya watu wa Peponi.
IQNA – Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Ulimwengu wa Kiislamu (ISESCO) limepokea nakala adimu ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono wa Abu al-Hasan Ali bin Hilal bin Abdul Aziz, mkaligrafia maarufu wa ulimwengu wa Kiislamu.
IQNA – Sherehe imefanyika katika Kambi ya Wakimbizi ya Al-Shati, magharibi mwa Gaza, kuadhimisha wanaume na wanawake 500 waliokamilisha kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Shambulio la kigaidi limewalenga waumini waliokuwa katika ibada ya Sala leo Ijumaa katika msikiti wa Imam Ali bin Abi Talib (AS) katika kitongoji cha Wadi al Dhahab katika mkoa wa Homs , Syria na kuuwa watu 5 na kujeruhi wengine 21.
IQNA – Mwanazuoni wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia kutoka Iraq anaamini kuwa tafiti mpya juu ya asili ya jina Buratha (mwana wa maajabu) na mawe ya ajabu ya Msikiti wa kihistoria wa Buratha huko Iraq zinaimarisha nadharia kwamba mahali pa kuzaliwa kwa Nabii Isa (Amani Iwe Juu Yake-AS-) si Beit Laham au Bethlehem, Palestina, bali Iraq.
IQNA-Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea kwenye msikiti ulioko katika Soko la Gamboru, mjini Maiduguri, katika Jimbo la Borno kaskazini-mashariki mwa Nigeria, lililopelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya Waislamu waliokuwemo msikitini humo.
IQNA – Mwanafikra na msanii Mkristo kutoka Lebanon amesema Nabii Isa na Mtume Muhammad (rehema na amani ziwashukie) waliona jukumu lao kuwa ni kusimamisha maadili na upendo wa kimungu.
IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu kwa Papa Leo wa XIV, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, akimpongeza kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Nabii Isa (amani iwe juu yake) na kuwadia Mwaka Mpya wa 2026.
IQNA – Wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Misri wamesoma aya za Qur’ani Tukufu kwa sauti ya pamoja kabla ya mechi dhidi ya Zimbabwe katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).