IQNA

Unyenyekevu wa Mohammad Salah wapelekea dada wawili Uingereza kusilimu

21:30 - August 25, 2021
Habari ID: 3474224
TEHRAN (IQNA)- Dada wawili nchini Uingereza wamesilimu baada ya kuvutiwa na unyenyekevu pamoja na maadili mema ya mchezaji soka maarufu wa Misri Mohammad Salah, ambaye ni fowadi wa klabu ya Liverpool katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Kwa mujibu wa taarifa, wasichana hao walisilimu katika safari yao hivi karibuni katika eneo la Aswan nchini Misri.

Dada hao wawili wawili, waliotambuliwa kama Amy na Nikki wanasema: “Tulivutiwa na maadili mema ya Waislamu barani Ulaya na pia unyenyekevu wa Mohammad Salah.”

Kwa maneno hayo, wasichana hao walibainisha mapenzi yao kwa Uislamu na furaha yao kwa kuukumbatia Uislamu maishani.

Tovuti ya Misri ya Al Youm Al Sabea imewanukuli dada hao wawili wakisema kuwa uamuzi wao wa kusilimu haukuwa chini ya mashinikizo bali wamechukua uamuzi huo baada ya kufanya utafiti wa kina.

Ammy na Nikki wanaishi Uingereza karibu na mji wa Liverpool na hutembelea Misri mara kwa mara.

Mohammad Salah ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Misri na anatajwa kuwa mchezaji wa tatu mwenye thamani kubwa zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza ambapo mkataba wake ni wenye thamani ya pauni milioni 100. Lakini pamoja na hayo ni mchezaji mneynyekevu na mwenye kuzingatia mafundisho ya Kiislamu maishani. Salah ni maarufu kwa kusujudu mara kwa mara baada ya kufunga bao.

Afisa wa utalii katika eneo la Aswan Abdeluaziz Al Idrisi anasema Amy na Nikki anasema dada hao wawili wana uelewa kamili wa nguzo tanzo za Uislamu na wanaamini pia ghaibu. Aidha anasema wamejifunza sura kadhaa za Qu’rani kwa lugha ya Kiarabu kama vile Al Fatiha, Al Ikhlas na Quraish.

captcha